Kugeuza baadhi ya sifa za Allaah kinyume na dhahiri yake

Swali: Anayesema kuwa sifa zipitishwe juu ya dhahiri yake isipokuwa pale ambapo kuna dalili ya kuzielekeza kinyume na dhahiri yake?

Jibu: Sifa zipo juu ya dhahiri yake na kutokana na maana yake inayolingana na Allaah. Lakini hakuna ajuaye namna yake isipokuwa Yeye. Tunajua ar-Rahmaan maana yake ni rehema, al-´Aziyz maana yake ni utukufu, al-´Aliym maana yake ni ujuzi, al-Istiwaa´ maana yake ni kuwa juu. Hata hivyo namna yake ndio yenye kutegemezwa kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Swali: Je, kuzigeuza sifa mbali na dhahiri yake kunahitaji dalili?

Jibu: Haijuzu kuzigeuza dhahiri yake isipokuwa kwa dalili inayoonyesha maana aliyoikusudia Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31625/هل-يجوز-صرف-بعض-صفات-الله-عن-ظاهرها
  • Imechapishwa: 11/11/2025