Swali: Tumejaribiwa katika nchi zetu kwa shule zenye mchanganyiko wa wavulana na wasichana. Mimi ni kijana mwenye kujitahidi katika dini na nimeajiriwa kuwa mwalimu katika mojawapo ya shule hizi za mchanganyiko, kwa sababu hakuna shule ya wavulana pekee katika nchi yetu. Lakini ipo shule nyingine iliyo mbali na nchi yangu ambayo inahitaji juhudi kubwa siku nzima na gharama nyingi ilihali mshahara wangu ni mdogo. Je, nibaki katika shule ya mchanganyiko au niombe kuhamishiwa shule ile nyingine hata kama italazimu kulipa pesa kwa wasimamizi?

Jibu: Angalia lipi lililo bora zaidi kwa moyo wako. Ikiwa wachelea juu ya nafsi yako, basi hama. Ikiwa unaona kuwa kuwepo kwako kunaleta maslahi kwa shule, kuwatia moyo katika kumtii Allaah, kuwahimiza wasichana kujisitiri, ukainamisha macho yako na ukafanya yale yanayolifaa ummah, basi endelea. Fanya lililo bora zaidi. Ikiwa unakhofia juu ya nafsi yako kwa sababu ya uwepo wa wasichana, basi mche Allaah, jihadhari na hama katika shule hiyo na wende shule nyingine au kazi nyingine. Ikiwa unaona kuwa kuwepo kwako shuleni kuna maslahi kwa waislamu na manufaa kwa waislamu. Aidha una uwezo wa kuinamisha macho yako, kuwaamrisha Hijaab na kujisitiri na kujitahidi pamoja na ndugu zako waliobaki katika jambo hili, basi wewe uko katika mpaka mkubwa miongoni mwa mipaka ya Uislamu. Basi mche Allaah katika hilo, fanya unaloweza katika kheri. Vinginevyo hama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2261/حكم-التدريس-في-المدارس-المختلطة
  • Imechapishwa: 09/01/2026