Kufunga ndoa kati ya sikukuu mbili

Swali: Je, inafaa kufunga ndoa kati ya ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa kwa sababu sisi huku Uturuki kuna msemo unaosema kwamba haifai kufunga ndoa kati ya sikukuu hizo mbili?

Jibu: Maneno haya ni batili na hayana msingi wowote. Inafaa kufunga ndoa katika wakati wote; katika Shawwaal, Dhul-Qa´adah, Dhul-Hijjah, Muharram, Swafar na miezi iliyosalia ya mwaka. Haijuzu dhana hii mbaya. Kwa mukhtaswari ni kwamba msemo unaosema kwamba haijuzu kufunga ndoa kati ya sikukuu hizo mbili au katika mwezi wa Swafar, siku ya jumatano au siku fulani yote ni batili. Allaah amefanya wasaa suala hili. Mwafikishwa ni yule aliyewafikishwa na Allaah ni mamoja kumefungwa ndoa katika Shawwaal, Swafar au miezi mingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11224/كم-عقد-النكاح-بين-العيدين
  • Imechapishwa: 29/04/2022