Swali: Bora kwa msafiri afunge au asifunge?
Jibu: Bora ni yeye kufanya lile ambalo ni lepesi zaidi. Ikiwa wepesi zaidi kwake ni kufunga, basi bora ni yeye kufunga. Na ikiwa wepesi zaidi kwake ni yeye kula, basi bora ni yeye kula. Endapo yote mawili yatakuwa ni sawa, basi bora ni kufunga. Kwa sababu hivi ndivo alikuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jengine ni kwa sababu mtu anaitakasa zaidi dhimma yake na inakuwa rahisi zaidi kwa mtu. Kwa sababu kulipa kunakuwa kugumu kwa mtu. Kwa hivyo mtu ana hali tatu:
1- Kuacha kufunga kunakuwa ndio wepesi zaidi kwake. Hivyo asifunge.
2- Kufunga kukawa ndio kwepesi zaidi kwake. Afunge.
3- Yote mawili yakiwa sawa basi bora ni yeye kufunga.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: I´laam-ul-Musaafiriyn, uk. 72
- Imechapishwa: 29/05/2019
Swali: Bora kwa msafiri afunge au asifunge?
Jibu: Bora ni yeye kufanya lile ambalo ni lepesi zaidi. Ikiwa wepesi zaidi kwake ni kufunga, basi bora ni yeye kufunga. Na ikiwa wepesi zaidi kwake ni yeye kula, basi bora ni yeye kula. Endapo yote mawili yatakuwa ni sawa, basi bora ni kufunga. Kwa sababu hivi ndivo alikuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jengine ni kwa sababu mtu anaitakasa zaidi dhimma yake na inakuwa rahisi zaidi kwa mtu. Kwa sababu kulipa kunakuwa kugumu kwa mtu. Kwa hivyo mtu ana hali tatu:
1- Kuacha kufunga kunakuwa ndio wepesi zaidi kwake. Hivyo asifunge.
2- Kufunga kukawa ndio kwepesi zaidi kwake. Afunge.
3- Yote mawili yakiwa sawa basi bora ni yeye kufunga.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: I´laam-ul-Musaafiriyn, uk. 72
Imechapishwa: 29/05/2019
https://firqatunnajia.com/kufunga-au-kutokufunga/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)