Swali: Vijana Aden wanawafunza wanawake misikitini pasi na pazia kati yao. Je, hilo linafaa?
Jibu: Ikiwa hakuna khatari ya mtihani na si mzungumzaji wala wanawake hawachelei mtihani na inahusiana tu na mawaidha, hapana vibaya. Ama kuhusu jambo la kufundisha, pengine muda utavyokuwa unaenda akaingia katika mtihani. Muda utakavyokuwa unaenda wakapata ujasiri wa kuuliza maswali. Huenda shaytwaan akamtelezesha. Imani ya mtu inapanda na kushuka.
Kuhusu dalili juu ya kwamba mawaidha yanafaa, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alienda siku ya ´iyd pamoja na Jaabir bin ´Abdillaah, ´Abdullaah bin ´Abbaas na Bilaal bin Abiy Rabaah (Radhiya Allaahu ´anhum) kuwapa kuwawaidhi wanawake. Ikiwa hakuna khatari ya fitina, basi hapana vibaya kama tulivyosema.
Kuhusu kufundisha, tunamchomnasihi ndugu yetu ni kwamba atafute kipaza sauti na spika na afundishe nyuma ya pazia. Hivo ni kwa sababu ya kusitokee fitina na ahifadhi usalama wa nyoyo.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 374-375
- Imechapishwa: 01/07/2025
Swali: Vijana Aden wanawafunza wanawake misikitini pasi na pazia kati yao. Je, hilo linafaa?
Jibu: Ikiwa hakuna khatari ya mtihani na si mzungumzaji wala wanawake hawachelei mtihani na inahusiana tu na mawaidha, hapana vibaya. Ama kuhusu jambo la kufundisha, pengine muda utavyokuwa unaenda akaingia katika mtihani. Muda utakavyokuwa unaenda wakapata ujasiri wa kuuliza maswali. Huenda shaytwaan akamtelezesha. Imani ya mtu inapanda na kushuka.
Kuhusu dalili juu ya kwamba mawaidha yanafaa, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alienda siku ya ´iyd pamoja na Jaabir bin ´Abdillaah, ´Abdullaah bin ´Abbaas na Bilaal bin Abiy Rabaah (Radhiya Allaahu ´anhum) kuwapa kuwawaidhi wanawake. Ikiwa hakuna khatari ya fitina, basi hapana vibaya kama tulivyosema.
Kuhusu kufundisha, tunamchomnasihi ndugu yetu ni kwamba atafute kipaza sauti na spika na afundishe nyuma ya pazia. Hivo ni kwa sababu ya kusitokee fitina na ahifadhi usalama wa nyoyo.
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 374-375
Imechapishwa: 01/07/2025
https://firqatunnajia.com/kufundisha-hadhira-ya-kike-bila-ya-pazia/