Kufukua makaburi yaliyokwishafanya muda mrefu

Swali: Yanayofanyika katika baadhi ya nchi wakati kaburi linapofanya muda mrefu na likawa mifupa wanaliweka kando na kuzika mwingine?

Jibu: Hapana, haifai kufanya hivyo. Inapasa kuwe na sehemu nyingi kwa kiasi cha haja ya watu na yasifukuliwe, kwa sababu maiti ni mwenye kuheshimiwa. Lakini ikiwa ni kwa ajili ya dharurah, basi dharurah zina hukumu zake. Kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Uhud akawazika wawili au watatu pamoja katika kaburi moja. Hapana vibaya ikiwa nchi ni ndogo na nafasi ni finyu, wakazikwa wawili au zaidi katika kaburi moja kwa sababu ya haja.

Swali: Vipi ikiwa hakubaki hata mfupa wowote?

Jibu: Hapana neno ikiwa ni kwa sababu ya haja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31121/ما-حكم-نبش-القبر-ليدفن-فيه-اخر
  • Imechapishwa: 03/10/2025