Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya zile sehemu za kina Thamuud kuwa ni mahali pa kutalii?
Jibu: Haijuzu kuingia sehemu kama hizo isipokuwa ikiwa kama mtu atalia. Kutokana na Hadiyth yenye kusema:
“Ikiwa hamkulia basi jilizeni.”
Haijuzu kuuingia isipokuwa kwa namna iliyotajwa katika Hadiyth:
“Msiingie nyumba za wale waliodhulumu isipokuwa ikiwa kama mtalia kwa kuchelea msije kupatwa na kilichowapata.”
Kwa ajili hii wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopita sehemu hiyo aliinamisha kichwa chake na akaharakisha mwendo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
- Imechapishwa: 15/05/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket