Swali: Kuna kijarida kwa jina ”Masaa-il Muhimmah fiyl-´Aqiydat-il-Islaamiyyah” ambacho ndani yake kumetajwa:
”Inajuzu kufanya Tawassul kwa mapenzi kwa ajili ya Allaah kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa mawalii Wake na kwa mapenzi yetu kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa mawalii Wake, kwa sababu mapenzi yetu kwao ni katika matendo mema. Tukasema kwa mfano:
”Ee Allaah! Kutokana na mapenzi Yako kwa Mtume Wako na kwa mawalii Wako basi tunusuru. Kutokana na mapenzi Yako kwa Mtume Wako na kwa mawalii Wako basi tuponye.”
Jibu: Ndio, hakuna tatizo kufanya Tawassul kwa mapenzi ya Allaah. Ni miongoni mwa sifa Zake (Jalla wa ´Alaa):
”Ee Allaah! Hakika mimi nafanya Tawassul Kwako kwa mapenzi Yako kwa mawalii Wako, kwa Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wenye kukutii. Ee Allaah! Hakika mimi nafanya Tawassul Kwako kwa mapenzi yetu kwa Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa mapenzi yetu Kwako na kwa mapenzi yetu kwa mawalii Wako wenye kukucha.”
Huku ni kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
”Allaah ana Majina mazuri kabisa, hivyo basi muombeni kwayo.”[1]
Mwanafunzi: Je, hili la pili si ni miongoni mwa matendo mema?
Ibn Baaz: Nini?
Mwanafunzi: Kwa mapenzi yangu kwa Mtume Wako si ni katika matendo mema?
Jibu: Hili ni tendo jema.
Swali: Lakini kwa mapenzi yake yeye juu ya Mitume na mawalii Wake?
Jibu: Kufanya Tawassul kwa mapenzi ya Allaah kwa mawalii Wake na kufanya Tawassul kwa mapenzi yetu kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yote ni sahihi. Hilo la kwanza ni kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah na la pili ni kufanya Tawassul kwa matendo yetu mema, mfano wa kisa cha watu wa pango.
[1] 07:180
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31060/ما-حكم-التوسل-بحب-الله-لرسوله-ولاولياىه
- Imechapishwa: 27/09/2025
Swali: Kuna kijarida kwa jina ”Masaa-il Muhimmah fiyl-´Aqiydat-il-Islaamiyyah” ambacho ndani yake kumetajwa:
”Inajuzu kufanya Tawassul kwa mapenzi kwa ajili ya Allaah kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa mawalii Wake na kwa mapenzi yetu kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa mawalii Wake, kwa sababu mapenzi yetu kwao ni katika matendo mema. Tukasema kwa mfano:
”Ee Allaah! Kutokana na mapenzi Yako kwa Mtume Wako na kwa mawalii Wako basi tunusuru. Kutokana na mapenzi Yako kwa Mtume Wako na kwa mawalii Wako basi tuponye.”
Jibu: Ndio, hakuna tatizo kufanya Tawassul kwa mapenzi ya Allaah. Ni miongoni mwa sifa Zake (Jalla wa ´Alaa):
”Ee Allaah! Hakika mimi nafanya Tawassul Kwako kwa mapenzi Yako kwa mawalii Wako, kwa Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wenye kukutii. Ee Allaah! Hakika mimi nafanya Tawassul Kwako kwa mapenzi yetu kwa Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa mapenzi yetu Kwako na kwa mapenzi yetu kwa mawalii Wako wenye kukucha.”
Huku ni kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
”Allaah ana Majina mazuri kabisa, hivyo basi muombeni kwayo.”[1]
Mwanafunzi: Je, hili la pili si ni miongoni mwa matendo mema?
Ibn Baaz: Nini?
Mwanafunzi: Kwa mapenzi yangu kwa Mtume Wako si ni katika matendo mema?
Jibu: Hili ni tendo jema.
Swali: Lakini kwa mapenzi yake yeye juu ya Mitume na mawalii Wake?
Jibu: Kufanya Tawassul kwa mapenzi ya Allaah kwa mawalii Wake na kufanya Tawassul kwa mapenzi yetu kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yote ni sahihi. Hilo la kwanza ni kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah na la pili ni kufanya Tawassul kwa matendo yetu mema, mfano wa kisa cha watu wa pango.
[1] 07:180
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31060/ما-حكم-التوسل-بحب-الله-لرسوله-ولاولياىه
Imechapishwa: 27/09/2025
https://firqatunnajia.com/kufanya-tawassul-kwa-mapenzi-ya-allaah-kwa-mtume-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket