Kufanya kazi kwenye kiwanda kinachotengeneza ndege za vita

Swali: Kuna kiwanda katika nchi ya kikafiri ambacho kinatengeneza ndege za vita kwa lengo la kujitetea au kushambulia. Je, inajuzu kwa muislamu kufanya kazi katika kiwanda kama hichi?

Jibu: Ikiwa kiwanda hichi kinatengeneza kwa ajili ya kuwapiga vita waislamu haijuzu kwa Muislamu kufanya kazi ndani yake. Katika hali hii itakuwa ni kushirikiana katika madhambi na uadui. Ama ikiwa haitengenezi kwa ajili ya kuwapiga vita waislamu, bali kwa madhumuni ya faida tu, inachukuliwa kuwa inajuzu. Haijuzu kwa muislamu kushiriki au kufanya kazi na kitu ambacho kinachangia kuwapiga vita waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo%20%20-%2021%20-%2008%20-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015