Kufanya Adhkaar kwa kufikiria tu

Swali: Imewekwa katika Shari´ah kufanya istighfari kwa moyo pasi na kutamka kwa ulimi?

Jibu: Haizingatiwi isipokuwa mpaka aitamke. Haitoshi kuisema kimyakimya ndani ya nafsi yake. Haizingatiwi kuwa ni isitighfari isipokuwa mpaka pale atapoutikisa ulimi wake. Ama kule kufikiria tu hakuzingatiwi kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (89) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D9%8A%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-08-07-1439.lite__0.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2018