Swali: Kuendelea juu ya dhambi ndogo kunaigeuza kuwa kubwa?

Jibu: Imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas ya kwamba kuendelea juu ya dhambi ndogo kunaifanya kuwa dhambi kubwa. Amesema:

“Hakuna dhambi kubwa pamoja na kutubia na wala hakuna dhambo ndogo pamoja na kuendelea.”

Kwa hivyo ni wajibu kujihadhari na kuendeleza dhambi. Ajizoweze kutubu na kuomba msamaha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23102/هل-الاصرار-على-الصغاىر-يجعلها-كباىر
  • Imechapishwa: 02/11/2023