Kuelekea Qiblah wakati wa kusoma Qur-aan

Swali: Vipi kuhusu kuelekea Qiblah wakati wa kusoma Qur-aan?

Jibu: Ikiwa ni kwa njia ya kufanyia kazi yale yaliyopokelewa katika baadhi ya Hadiyth:

”Vikao bora ni vile vinavyoelekewa Qiblah.”[1]

kwa mwelekeo huo, basi nakuna kizuizi ya kwamba muislamu wakati wa kusoma kwake Qur-aan akaelekea Qiblah. Lakini kwa mantiki ya kwamba ni moja miongoni mwa adabu kwa njia ya kwamba asipoifaya mwingine basi asikemewe. Kwa sababu sio miongoni mwa mambo aliyomafaradhishia juu yake.

[1] at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw” (03/25/2354). Tazama ”as-Swahiyhah” (2645) na ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (3085)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 39
  • Imechapishwa: 01/07/2022