Kuelekea Qiblah cha sawa ndani ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya imamu anayeswali kinyume na Qiblah mahali pa kuswalia pa treni? Alipokuja kujua kuwa anaswali kusipokuwa Qiblah akaelekea Qiblah bila ya kukata swalah yake au kuirudi?

Jibu: Hakuna matatizo. Alifanya aliwezalo na kuanza kuswali kusikokuwa Qiblah. Baada ya hapo akaona mwelekeo sahihi na akaelekea huko. Swalah yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017