Kudumu na Qunuut katika Fajr kwa hoja ya majanga yanayowapata waislamu

Swali: Baadhi ya watu wanasema kwamba waislamu sasa wanahitaji msaada wa kudumu na hivyo basi du´aa katika Fajr inakuwa kwa mtindo wa kudumu?

Jibu: Hapana, si jambo linalopaswa kufanywa isipokuwa kama yametokea matukio makubwa. Ama uadui wa makafiri dhidi ya waislamu, umekuwepo na unaendelea tangu zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Vipi kuhusu mitetemeko ya ardhi na milipuko ya volcano?

Jibu: Hapana, jambo linalojulikana ni kushuka kwa adui kafiri.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27040/هل-يداوم-على-القنوت-في-الفجر-بحجة-كثرة-النوازل
  • Imechapishwa: 23/03/2025