Swali: Je, inasihi kusema kwa ambaye anaendelea juu ya maasi kwamba anayo dosari katika ´Aqiydah?
Jibu: Akiendelea hatosamehewa. Allaah amesema:
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ
“Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao, basi humdhukuru Allaah wakaomba msamaha kwa madhambi yao. Na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah? Na hawaendelei katika waliyoyafanya ilihali wanajua.”[1]
Ni lazima kutodumu. Allaah ameweka sharti la msamaha kuwa asidumu. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:
”Swalah tano, ijumaa moja mpaka ijumaa na Ramadhaan mpaka Ramadhaan ni kafara ya yaliyo kati yao iwapo yataepukwa madhambi makubwa.”
Hili linaenda sambamba na maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا
“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[2]
Kwa hiyo ameweka sharti katika kusamehewa na kuingia Peponi kwamba mtu aepuke madhambi makubwa.
Swali: Mwenye kusema kuwa muislamu anayedumu katika maasi – nayo ni madhambi makubwa – asiitwe muumini na kwamba aitwe muislamu tu?
Jibu: Huitwa muislamu na huitwa muumini mwenye imani pungufu.
[1] 03:135
[2] 04:31
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31044/هل-الاصرار-على-المعاصي-خلل-في-الاعتقاد
- Imechapishwa: 26/09/2025
Swali: Je, inasihi kusema kwa ambaye anaendelea juu ya maasi kwamba anayo dosari katika ´Aqiydah?
Jibu: Akiendelea hatosamehewa. Allaah amesema:
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ
“Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao, basi humdhukuru Allaah wakaomba msamaha kwa madhambi yao. Na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah? Na hawaendelei katika waliyoyafanya ilihali wanajua.”[1]
Ni lazima kutodumu. Allaah ameweka sharti la msamaha kuwa asidumu. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:
”Swalah tano, ijumaa moja mpaka ijumaa na Ramadhaan mpaka Ramadhaan ni kafara ya yaliyo kati yao iwapo yataepukwa madhambi makubwa.”
Hili linaenda sambamba na maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا
“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[2]
Kwa hiyo ameweka sharti katika kusamehewa na kuingia Peponi kwamba mtu aepuke madhambi makubwa.
Swali: Mwenye kusema kuwa muislamu anayedumu katika maasi – nayo ni madhambi makubwa – asiitwe muumini na kwamba aitwe muislamu tu?
Jibu: Huitwa muislamu na huitwa muumini mwenye imani pungufu.
[1] 03:135
[2] 04:31
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31044/هل-الاصرار-على-المعاصي-خلل-في-الاعتقاد
Imechapishwa: 26/09/2025
https://firqatunnajia.com/kudumu-katika-maasi-ni-dosari-katika-aqiydah-ya-mtu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket