Kuchukua zakaah au mkopo kwa ajili ya kuongeza mke

Swali: Kuchukua mkopo kwa ajili ya kuoa mke wa pili na wa tatu?

Jibu: Hapana vibaya. Ikiwa ni mlipaji hapana vibaya akachukua mkopo na kuoa. Ikiwa ni mlipaji na ni mwenye kufanya sababu, anafanya biashara au amejiajiri mwenyewe.

Swali: Je, achukue kutoka katika zakaah?

Jibu: Hapana vibaya akihitaji. Ikiwa analo deni au hana chochote apewe katika zakaah kiasi atachoweza kuoa kwacho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23853/حكم-من-يستدين-ليتزوج-الثانية-والثالثة
  • Imechapishwa: 19/05/2024