Kuchukua asilimia ya pesa kadhaa katika miradi ya mashirika ya kazi za Ummah

Swali: Mimi nafanya kazi katika ofisi ya ad-Da´wah wal-Irshaad. Ofisi hunipa asilimia kumi kwa kila pesa ninayopata kwa ajili ya ofisi. Je, pesa hii ninayopewa haina neno?

Jibu: Hili linahitajia upammbanuzi. Kilicho karibu zaidi ni kwamba hawamiliki kukupa chochote ikiwa hiyo ni michango. Isipokuwa ikiwa michango hiyo sio kwa ajili ya Da´wah. Michango hiyo inatakiwa iwe mafungu mawili:

1- Fungu la kwanza kwa ajili ya haja mbalimbali za ofisi na kwa ajili ya walinganizi.

2- Fungu lingine kununua vitabu au kitu maalum.

Hastahiki kupewa kitu katika fungu hili la pili. Hakuna neno ikiwa michango hiyo ikiwa ni kwa ajili ya ofisi na mahitajio yake mbalimbali samani ya ofisi kama vile viti, wafanyikazi na mshahara wa wafanyikazi. Kusema achukue kutoka katika michango yote ni jambo linahitajia upambanuzi. Kwa sababu watu wengi wanajitolea michango yao lakini wamekusudia kwayo Da´wah. Kwa mfano wanajitolea kwa ajili ya waalimu au kitu maalum. Haitakikani kuchukua isipokuwa kutoka katika ile michango ilioenea.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 26/06/2020