Kuchelewesha ´Ishaa kwa sababu ya kutazama TV

Swali: Ni yepi maoni yako juu ya yule mwenye kuchelewesha swalah ya ´Ishaa katika Ramadhaan kwa sababu ya kutazama musalsal?

Jibu: Amekosea kosa kubwa. Kwa sababu haifai kwa mtu kuchelewesha swalah ya mkusanyiko, si katika Ramadhaan wala miezi mingine. Khaswakhaswa kwa kuzingatia kwamba anatazama musalsal ambazo huenda zikawa mbaya kama hali ilivyo mara nyingi. Ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na ajitahidi kumtii Allaah (Ta´ala) katika mwezi huu. Kwa sababu hajui kama utamrudilia au hapana. Ni watu wangapi ambao Ramadhaan hazikuwarudilia? Ni watu wangapi ambao wametamani Ramadhaan na wakafa kabla ya kufika hata ile siku ya kwanza? Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah kuanzia hivi sasa na aazimie kuukubali mwezi wa Ramadhaan kwa hima ya hali ya juu na azima ya kweli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1571
  • Imechapishwa: 07/03/2020