Kuchanganya visomo vingi katika Suurah moja

Swali: Vipi kuhusu kusoma katika swalah kwa kuchanganya kati ya visomo saba katika Suurah moja?

Jibu: Kinachonidhihirikia ni kwamba haipaswi kufanya hivyo. Anachotakiwa ni yeye kusoma kisomo kimoja. Lakini midhali msahafu upo mikononi mwa watu, ni bora mtu asome kulingana na yaliyomo kwenye msahafu ulio na watu ili kuepuka migogoro na mivutano. Hata hivyo ikiwa ni kwa madhumuni ya kufundisha watu visomo saba au visomo kumi, hapana vibaya kwa sababu hiyo ni sehemu ya kufundisha na ina nafasi pana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24842/حكم-الجمع-بين-عدة-قراءات-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 20/12/2024