Swali: Ni ipi hukumu ya kuzika kucha na nywele baada ya kuzikata?
Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa kuzika nywele na kucha ndio vizuri na bora zaidi. Hayo yamepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Si sawa kuyaacha sehemu ya wazi au kuyatupa katika mahali kunakopelekea katika dhambi.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/132)
- Imechapishwa: 30/06/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kujizuia kukata nywele, kucha na ngozi Dhul-Hijjah kwa aliyenuia kuchinja
Ukiingia mwezi wa Dhul-Hijjah na yeye amenuia kuchinja basi asikate chochote katika nywele wala kucha zake mpaka achinje. Hili linamuhusu yeye pekee. Kuhusu familia yake hapana vibaya kwao. Linamuhusu yeye pekee aliyejitolea pesa ya kichinjwa. Yeye ndiye asikate chochote katika nywele wala kucha zake mpaka akishachinja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi…
In "Kukata nywele, ngozi na kucha"
Kutokata nywele wala kucha Dhul-Hijjah kwa atakayechinja
Yule aliyekusudia kuchinja katika ´Iydh-ul-Adhwhaa basi zinapoingia tu zile siku [kumi za mwanzo] za Dhul-Hijjah basi haifai kwake kukata chochote katika nywele na kucha zake isipokuwa mpaka baada ya kuchinja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Zitapoingia zile siku kumi [za Dhul-Hijjah] na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asichukue/asikate…
In "Kukata nywele, ngozi na kucha"
Ni haramu kukata kucha kwa ambaye atachinja
Swali: Nimesikia kwa baadhi ya watu wanasema kwamba haifai kwa mtu kukata kucha zake katika yale masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah. Je, niliyosikia ni kweli? Jibu: Ikiwa anataka kuchinja basi haifai kwake kukata kucha zake, nywele zake wala chochote katika mwili wake mpaka pale atapochinja baada ya kuingia mwezi.…
In "Kukata nywele, ngozi na kucha"