Swali: Ni ipi hukumu ya kuapa kwa talaka kama kusema “ni juu yangu talaka”?

Jibu: Haijuzu. Ni miongoni mwa Bid´ah. Akiapa kwa talaka na akaikusudia basi inapita kwa maafikiano. Na ikiwa makusudio yake ni ima kusadikisha, kukadhibisha, kusisitiza au kukataza jambo, hapo ndipo wanachuoni wametofautiana. Maimamu wanne wanaona kuwa ni yenye kupita. Shaykh-ul-Islaam na kikosi cha wanachuoni wengine wanaona kuwa hukumu yake ni kama yamini. Waulizwe watoa fatwa wakati wa haja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 31/01/2021