Kuapa kwa haramu na talaka

Swali: Vipi kwa ambaye anaapa kwa haramu na talaka?

Jibu: Haijuzu. Asiape kwa haramu wala talaka. Haijuzu akisema ni haramu kwangu kitu fulani, kwa sababu haifai kwake kuharamisha kile alichohalalisha Allaah. Lakini akisema ni lazima kwangu kuacha, sio kiapo kwa mujibu wa Shari´ah. Ni kiapo upande wa lugha na desturi  ya wanazuoni. Kiapo kinakuwa kwa (الألف), (الهاء), (الواو), (التاء) na (الباء). Ama kusema ni lazima kwangu kuacha, kwa mujibu wa wanazuoni ni yamini, kwa sababu ndani yake kuna kutilia mkazo.

Swali: Kwa hiyo mke haachiki?

Jibu: Hapana, kwa mujibu wa maoni sahihi inakuwa yenye kuntundikwa kwa mujibu wa nia yake; ikiwa alikusudia kusisitiza na kukataza basi inakuwa na hukumu moja kama kiapo, na kama alikusudia talaka ipite basi imepita.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23953/حكم-الحلف-بالحرام-والطلاق
  • Imechapishwa: 03/08/2024