Swali: Ni ipi hukumu ya kuapa kwa tamko lisemalo

“Kwa haki ya Allaah.”?

Je, kiapo hiki kinahesabiwa kuwa ni shirki kwa Allaah hata kama hakukusudia?

Jibu: Hapana. Haifai kuapa kwa haki ya Allaah. Anaapa kwa Allaah kwa kusema:

والله، بعزة الله، والرحمن الرحيم، والقادر على كل شيء، ورب العالمين، والذي نفسي بيده

”Naapa kwa jina la Allaah, naapa kwa utukufu wa Allaah, naapa kwa Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, naapa kwa Muweza juu ya kila kitu, naapa kwa Mola wa walimwengu wote au naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake.”

Haifai kuapa kwa haki ya Allaah, kwa sababu haki ya Allaah juu yetu ni kumtukuza na kumtii. Kumtukuza na kumtii ni katika matendo yetu, nayo ni katika matendo ya viumbe. Haki Yake juu yetu ni kumpwekesha, kumtii, kumtukuza, kumpwekesha kwetu, kumtukuza Kwake na kumtii Kwake ni katika matendo yetu ambayo ni kiumbe. Maana yake inarudi kuwa ni kuapa kwa viumbe. Basi hilo halisihi. Kiapo hakiwi isipokuwa kwa Allaah peke Yake au kwa majina na sifa Zake (Jalla wa ´Alaa).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1812/حكم-الحلف-بحق-الله
  • Imechapishwa: 04/07/2026