Kuanza kwa chakula inahusiana na chakula cha jioni peke yake?

Swali: Kuanza kwa chakula inahusiana na chakula cha jioni peke yake?

Jibu:

”Kunapotengwa… ”

Ni jambo lenye kuenea chakula cha jioni na chengine. Kwa ajili hiyo Hadiyth ya ´Aaishah inasema:

”Hakuna swalah kunapotengwa chakula wala wakati anajaribu kuzuia haja kubwa na ndogo.”

Kunaingia pia chakula cha mchana wakati kunapotengwa chakula wakati wa adhaana ya ´Aswr au adhaana ya Dhuhr.

Swali: Wako inasemekana kuwa jambo hilo linahusu kipindi cha wakati wa njaa na si leo?

Jibu: Hapana, amekosea aliyesema hivo. Ameyasema kutoka mfukoni mwake. Lakini haitakikani jambo hilo lifanywe ndio mazowea na watu wakachukulia ndio udhuru. Hapana. Hilo likitokea bahati mbaya. Ama kukusudia na kuwaambia watu watenge chakula wakati kunapoadhiniwa maana yake ni kwamba hataki kuswali swalah ya mkusanyiko. Hilo ni pale linapotokea bahati mbaya ambapo chakula kikaletwa kwa ajili ya wageni na ametengewe yeye bila yeye kukiomba. Katika hali hii ataanza kula kwanza ili moyo wake usifungamane nacho. Malengo ni ili aje kuswali hali ya kuwa na unyenyekevu, moyo wake umehudhuria na akiwa na utulivu. Asifanye ndio mazowea kunatengwa chakula wakati wa swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24001/هل-تقديم-الطعام-على-الصلاة-خاص-بالعشاء
  • Imechapishwa: 17/08/2024