Swali: Je, kuamrisha mema na kukataza maovu kunahesabiwa kuwa ni nguzo ya sita ya Uislamu?
Jibu: Si nguzo ya sita. Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa ni ya sita, wakaifungamanisha na shahaadah mbili, swalah, zakaah, swawm na hajj. Wameita nguzo ya sita kwa sababu ya ukubwa wa jambo lake na faida yake kubwa. Hakika ni wajibu mkubwa na faradhi tukufu juu ya waislamu. Lakini si nguzo ya sita, kwa sababu watu hawatungi Shari´ah. Anayetunga Shari´ah ni Allaah kupitia kwa Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza wazi kwamba Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano. Kwa hivyo hakuna yeyote mwenye haki ya kuongeza juu ya hilo. Jambo hili ni jukumu la Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2136/حكم-اعتبار-الامر-بالمعروف-والنهي-عن-المنكر-ركنا-سادسا-للاسلام
- Imechapishwa: 27/03/2026
Swali: Je, kuamrisha mema na kukataza maovu kunahesabiwa kuwa ni nguzo ya sita ya Uislamu?
Jibu: Si nguzo ya sita. Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa ni ya sita, wakaifungamanisha na shahaadah mbili, swalah, zakaah, swawm na hajj. Wameita nguzo ya sita kwa sababu ya ukubwa wa jambo lake na faida yake kubwa. Hakika ni wajibu mkubwa na faradhi tukufu juu ya waislamu. Lakini si nguzo ya sita, kwa sababu watu hawatungi Shari´ah. Anayetunga Shari´ah ni Allaah kupitia kwa Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza wazi kwamba Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano. Kwa hivyo hakuna yeyote mwenye haki ya kuongeza juu ya hilo. Jambo hili ni jukumu la Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2136/حكم-اعتبار-الامر-بالمعروف-والنهي-عن-المنكر-ركنا-سادسا-للاسلام
Imechapishwa: 27/03/2026
https://firqatunnajia.com/kuamrisha-mema-ni-nguzo-ya-sita/