Kuamrisha mema na kukataza maovu ni kazi ya mwanaume na mwanamke

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu…”

Katika Aayah hii kuna dalili yenye kuonesha kuwa kazi ya kuamrisha mema na kukataza maovu sio kwa wanaume peke yao. Ni lazima kwao kuamrisha mema na kukataza maovu. Lakini hata hivyo inatakiwa iwe kwenye uwanja wa wanawake wenzake. Haitakiwi iwe katika mkusanyiko na masomo ya wanaume. Inatakiwai we katika uwanja na mkusanyiko wa wanawake kama katika siku za harusi, masomo na kadhalika. Mwanamke akiona maovu ayakataze. Na akiona jambo la wajibu linatumiwa vibaya aliamrishe. Kuamrisha mema na kukataza maovu ni jambo la wajibu kwa kila muumini:

يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

“… wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanasimamisha swalah na wanatoa zakaah na wanamtii Allaah na Mtume Wake – hao Allaah atawarehemu. Kwani hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hekima.”[2]

[1] 09:71

[2] 09:71

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/411)
  • Imechapishwa: 30/07/2025