10Sasa mwanamume anayefanya uzinzi na mke wa mwanamume mwingine ni mwanamume anayefanya uzinzi na mke wa mwenzake lazima auawe, mwanamume huyo mzinzi na vilevile mwanamke huyo mzinzi. 11Na mwanamume anayelala na mke wa baba yake ameufunua uchi wa baba yake. Lazima wote wawili wauawe. Damu yao wenyewe iko juu yao. 12Na mwanamume akilala na binti-mkwe wake, lazima wote wawili wauawe. Wamevunja jambo la asili. Damu yao wenyewe iko juu yao. 13Na mwanamume akilala na mwanamume sawa na vile mtu anavyolala na mwanamke, wote wawili wamefanya jambo lenye kuchukiza. Lazima wauawe. Damu yao wenyewe iko juu yao. 14Na mwanamume akimchukua mwanamke pamoja na mama yake, ni mwenendo mpotovu. Watamteketeza yeye na wao katika moto; ili mwenendo mpotovu usiendelee katikati yenu.
15Na mwanamume akimpa mnyama shahawa yake imtokayo, lazima auawe, nanyi mtamuua mnyama huyo. 16Na mwanamke akimkaribia mnyama yeyote ili kuungana naye, mtamuua mwanamke huyo na mnyama huyo. Lazima wauawe. Damu yao wenyewe iko juu yao.
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Walawi 20:10
- Imechapishwa: 12/01/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kupigwa mawe ndani ya Biblia
22Mwanamume akifumaniwa na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanamume na mwanamke, lazima wauawe. Ndivyo mtakavyokomesha uovu huo miongoni mwenu. 23Mwanamume akimkuta msichana aliyechumbiwa, akalala naye, 24mtawatoa wote wawili nje ya mji na kuwapiga mawe mpaka wafe. Msichana huyo lazima auawe kwa kuwa hakupiga kelele asaidiwe ingawa alikuwa mjini; naye mwanamume…
In "Uzinzi katika Biblia"
Machafu na madhambi nchini katika Biblia
19Kamwe usilale na mwanamke awapo mwezini. 20Kamwe usilale na mke wa jirani yako na hivyo kujitia mwenyewe najisi naye. 21Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. 22Kamwe usilale na mwanamume mwenzio kana kwamba ni…
In "Uzinzi katika Biblia"
Mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke ila mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume
2Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni. 3Lakini napenda pia mjue kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume na mwanamume ni kichwa cha mkewe na […]. 4Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo. 5Na mwanamke akisali au kutangaza ujumbe…
In "Mwanamke katika Biblia"