Kuachia mikono ndani ya swalah inachukiza

Swali: Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu mtukufu X – Allaah amjaalie tawfiyq katika kila kheri na amzidishie elimu na imani, Aamiyn.

سلام عليكم ورحمة الله وبركاته

”Amani, rehema za Allaah na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

Umeuliza kuhusu kuachia mikono wakati wa kusimama katika swalah?

Jibu: Hili ni jambo linalochukiza. Sunnah ni kuikusanya mikono, kuiweka juu ya kifua na kuweka mkono wa kulia juu ya kiganja cha kushoto, kifundo cha mkono na sehemu ya mkono. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Sahl bin Sa´d, Waa-il bin Hujr na Hulayb at-Twaa-iy yanayofahamisha hivo.

Kuhusu kuachia mikono, hakuna dalili juu yake. Bali ni kinyume na Sunnah. Lakini haifai kufanya ukali katika jambo hili, bali kilichosuniwa ni kufundisha Sunnah kwa upole na hekima.

والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/242)
  • Imechapishwa: 02/03/2026