Kuacha kuswali msikitini kwa hoja ya nguo chafu

Swali: Nina mwenzangu kazini (karakana ya magari) ninamwita kwenda kuswali, lakini anakataa kwa hoja kwamba nguo zake si safi na ni vigumu kwake kuzibadilisha na kwamba ataswali atakaporudi makazi yake. Ni ipi hukumu ya kitendo chake hichi?

Jibu: Ni wajibu kwa huyo mwenzako aliyetajwa kuswali pamoja na mkusanyiko. Haijuzu kwake kuchelewesha swalah mpaka arudi nyumbani kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote mwenye kusikia mwito kisha asiutikie, basi hana swalah isipokuwa kwa udhuru.” Akaulizwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): ”Udhuru ni nini?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

Udhuru ni maradhi na mfano wake. Ama kusema kwamba nguo ni chafu sio udhuru. Lakini kama ziko na najisi, basi ni wajibu kwake kuziosha au kuzibadilisha kwa nguo zilizo twahara. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) awaongoze wote.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/121)
  • Imechapishwa: 02/03/2026