Swali: Khofu ilio kwangu ni kule kutokujua sharti za kupangusa juu ya khufuu. Wakati mwingine yananitokea baadhi ya makosa na swalah zangu zinakuwa baada ya muda kuisha pamoja na kuamini na kuitakidi kuwa inajuzu kupangusa juu yake. Hilo lilinifanya nikaanza kuacha kupangusa juu ya khufuu. Je, kitendo changu hichi kina makosa ya wazi?

Jibu: Kitendo hichi kina makosa ya wazi. Ingelikuwa mtu anaacha ´ibaadah kwa sababu zinamtatiza basi tungemwambia ikiwa unasahau katika swalah zako acha kuswali. Nasaha yangu kwa kwa ndugu huyu na watu mfano wake wafuate Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia al-Mughiyrah bin Shu´bah:

“Ziache.”

Baada ya hapo akapangusa juu yake. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu baada yangu.”

Lakini unaweza kujifanyia wepesi kwa kuvaa soksi kuanzia wakati wa fajr na ukazivua wakati wa kulala. Katika hali hiyo hutotatizika. Kwa sababu ukizivaa wakati wa fajr na ukapangusa wakati wa kulala utakuwa ule muda wako haujaukamilisha na hutosahau. Katika hali hii unalala hali ya kuwa miguu yako iko wazi na unapata utulivu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (23)
  • Imechapishwa: 03/01/2019