Swali: Mwaka uliopita nilitaka kuchinja ng´ombe lakini nikaambiwa kuwa kondoo ndio bora zaidi. Je, kumepokelewa Hadiyth inayofahamisha kuwa kondoo ndio bora zaidi?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja kondoo wawili. Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo. Akiweza kuchinja kondoo ndio bora. Lakini ni sawa pia akimchinja ngamia au ng´ombe. Maswahabah walichinja mara hawa na mara hawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja Hadiy katika hijjah ya kuaga ngamia mia kwa ajili ya kujitolea tu. Kwa hiyo akichinja ngamia au ng´ombe ni sawa. Hata hivyo kondoo ndio bora zaidi akiweza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12102/الدليل-على-افضلية-الاضحية-بالكبش
  • Imechapishwa: 13/06/2024