Ni mnyama yupi katika Udhhiyah bora kumchinja? II

Swali: Bora katika ´Iyd-ul-Adhwhaa ni kuchinja kondoo au ng´ombe?

Jibu: Kuchinja kondoo ndio bora. Hakuna neno mtu akichinja ng´ombe au ngamia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo wawili. Siku ya hijjah ya kuaga alichinja ngamia mia. Tunachotaka kusema ni kwamba bora ni mtu kuchinja kondoo. Yule mwenye kuchinja ng´ombe au ngamia kila mmoja wakachangia watu saba yote ni mazuri na hakuna neno.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/43)
  • Imechapishwa: 25/07/2020