Swali: Je, kuna kiwango kati ya matembezi mawili ya kuyatembelea makaburi?

Jibu: Hakuna kiwango. Lakini asiwe siku zote ni mwenye kuyatembelea.

Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuyatembelea kwenye masikukuu baada ya swalah ya idi?

Jibu: Hapana. Hakuwekwi kikomo siku ya ijumaa wala katika masikukuu. Pale itapomuwepesikia atayatembelea. Haijalishi kitu ni siku gani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (15) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-24-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2019