Swali: Vipi kuhusu mtu kuitwa kwa sifa ya Allaah?

Jibu: Ni jambo linahitaji upambanuzi. Kuna majina ambayo anaitwa Allaah pekee. Kama mfano wa Muumba wa waumba (خالق الخلق), Muumbaji wa kila kitu (الخلَّاق) na Mwenye kuruzuku (الرزَّاق). Kuna majina ambayo inafaa kwa viumbe kuitwa kayo. Mfano wa majina hayo ni Mshindi (العزيز), Mzuri (الجميل), Mwenye huruma (الرحيم) na mfano wake:

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Kwa hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe. Yanamuhuzunisha yale yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. Ni mpole na mwenye huruma kwa waumini.” (09:128)

Swali: Inafaa kuitwa ´Abdul-Jaliyl?

Jibu: Hilo ni jina la Allaah. Ni jina tukufu. Jaliyl ni katika majina ya Allaah. Ni kama ´Abdul-Kariym.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24810/حكم-التسمي-بصفة-من-صفات-الله
  • Imechapishwa: 17/12/2024