Hadiyth hii kubwa ambapo Mu´aadh anabainisha yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyomtuma kwa watu wa Yemen kuna faida zifuatazo:

Kitu cha kwanza wanacholinganiwa watu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki ispokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Hili ndio jambo la kwanza kabla ya kila kitu. Unapowaendea makafiri kuwalingania usianze kwa kuwaambia waache pombe, uzinzi na ribaa. Hili ni kosa. Anza kwa msingi wa misingi kwanza kisha ndio uende kwenye tanzu. Kitu cha kwanza unachotakiwa kulingania ni katika Tawhiyd na ujumbe; washuhudie ya kwamba  hapana mungu wa haki ispokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Halafu baada ya hapo mbainishie nguzo zingine za dini kisha ufuatishie lililo muhimu zaidi ya lingine na kuteremka.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/502-503)
  • Imechapishwa: 10/09/2025