Swali: Kuna mtu amefiwa na baba yake. Bwana mmoja akampa pesa 100 ili asome Qur-aan na thawabu zimwendee baba yake. Ni ipi hukumu ya chukua pesa hizi? Thawabu zinamfikia yule maiti?
Jibu: Hiyo ni Bid´ah. Haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipofariki msichana wake Zaynab, mtoto wake wa kiume kutoka kwa Maariyah, Hamzah, ´Uthmaan bin Madh´uun na jopo la Maswahabah wengine ya kwamba alipeana pesa ili watu wasome Qur-aan kwa kumkusudia fulani. Huo ni ujanja wa kuchukua pesa za watu kwa batili.
Kuhusu Hadiyth inayosema:
“Hakika ambacho kina haki zaidi ya kuchukuliwa malipo ni Kitabu cha Allaah.”
ni Swahiyh. Hata hivyo mtu afupizike kutokana na sababu yake kutokana na dalili nyenginezo ambazo ni katika matabano.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 326
- Imechapishwa: 29/04/2025
Swali: Kuna mtu amefiwa na baba yake. Bwana mmoja akampa pesa 100 ili asome Qur-aan na thawabu zimwendee baba yake. Ni ipi hukumu ya chukua pesa hizi? Thawabu zinamfikia yule maiti?
Jibu: Hiyo ni Bid´ah. Haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipofariki msichana wake Zaynab, mtoto wake wa kiume kutoka kwa Maariyah, Hamzah, ´Uthmaan bin Madh´uun na jopo la Maswahabah wengine ya kwamba alipeana pesa ili watu wasome Qur-aan kwa kumkusudia fulani. Huo ni ujanja wa kuchukua pesa za watu kwa batili.
Kuhusu Hadiyth inayosema:
“Hakika ambacho kina haki zaidi ya kuchukuliwa malipo ni Kitabu cha Allaah.”
ni Swahiyh. Hata hivyo mtu afupizike kutokana na sababu yake kutokana na dalili nyenginezo ambazo ni katika matabano.
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 326
Imechapishwa: 29/04/2025
https://firqatunnajia.com/kisomo-cha-qur-aan-juu-ya-roho-ya-baba-aliyefariki/