Swali: Je, kisomo cha imamu ndio kisomo cha maamuma?

Jibu: Imekuja katika Hadiyth:

“Mwenye kuswali nyuma ya imamu basi kisomo chake ndio kisomo chake.”

Lakini Hadiyth hii ni dhaifu.

Wanachuoni wametofautiana juu ya masuala haya. Wanachuoni wengi wanaona kuwa kisomo cha al-Faatihah cha imamu katika swalah za kusoma kwa sauti kinatosha. Yapo maoni mengine ya wanachuoni yanayosema kwamba al-Faatihah imevuliwa. Hayo ni kutokana na yale yaliyopokelewa katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Huenda nyinyi mnasoma nyuma ya imamu wenu?” Wakasema: “Ndio.” Akasema: “Msisome isipokuwa tu mama wa Qur-aan. Kwani hana swalah yule ambaye hakuisoma.”

Kwa hivyo haya yanayavua maneno yake:

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Inaposomwa Qur-aan basi isikilizeni na nyamazeni kimya ili mpate kurehemewa.” (07:204)

Imepokelewa katika Hadiyth:

“Ataposoma basi nyamazeni.”

Katika hayo kunavuliwa Suurah “al-Faatihah”. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hana swalah yule ambaye hakuisoma.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 28/09/2019