Swali: Je, kisomo cha imamu kinamtosheleza maamuma katika swalah za kusoma kwa sauti?
Jibu: Hakimtoshelezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hana swalah yule ambaye hakusoma ufunguzi wa Kitabu.”[1]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:
“Pengine nyinyi mnasoma nyuma ya imamu wenu.” Wakasema: “Ndio, kwa haraka, ee Mtume wa Allaah.” Ndipo akasema: “Msifanye hivo isipokuwa kwa ufunguzi wa Kitabu, kwani hana swalah yule ambaye hakusoma ufunguzi wa Kitabu.”[2]
Kwa hivyo amewaruhusu wasome ufunguzi wa Kitabu. Kwa hivyo kusoma Suurah “al-Faatihah” ni lazima katika kila Rak´ah. Napendekeza msome kitabu ”al-Qiraa-ah khalf al-Imaam” cha Imaam al-Bukhaariy na ”al-Qiraa-ah khalf al-Imaam” cha Imaam al-Bayhaqiy.
Kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):
وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
“Inaposomwa Qur-aan basi isikilizeni na nyamazeni kimya ili mpate kurehemewa.”[3],
ash-Shawkaaniy amesema kuwa Aayah ni maalum juu ya “al-Faatihah”.
Kuhusu Hadiyth ya Abu Muusa al-Ash´ariy kwa Muslim inayosema:
“Na anaposoma, basi nyamazeni.”[4]
ni ziada yenye kasoro na iliyokosolewa, kama alivosema ad-Daaraqutwniy na an-Nawawiy akaafikiana naye. Vivyo hivyo kuhusu Hadiyth ya Abu Hurayrah kwa Abu Daawuud inayosema:
“Na anaposoma, basi nyamazeni.”
Kuna maoni tofauti juu ya Abu Hayyaan Sulaymaan al-Ahmar. Maoni yenye nguvu zaidi ni kwamba ni mnyonge. Hakukuthibiti kitu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallama).
Kuhusu Hadiyth:
“Yule aliye na imamu [basi atambue kuwa] kisomo cha imamu ndio kisomo chake.”[5]
amesema Haafidhw Ibn Kathiyr:
“Imepokelewa kupitia njia nyingi na hakuna yeyote iliyothibiti.”[6]
Ni kweli kwamba Ahmad ameipokea katika “al-Musnad” kwa cheni ya wapokezi ambayo udhahiri wake ni nzuri, lakini kupitia kwenye ”al-Qiraa-ah khalf al-Imaam” imethibiti kuwa jina la Jaabir bin al-Yaziyd al-Ju´fiy liliachwa katika cheni ya wapokezi. Alikuwa ni mwongo. Katika kitabu hichocho Imaam al-Bukhaariy amesema endapo Hadiyth hiyo ingelikuwa imesihi, basi isingelikuwa na maana ya kutosoma ufunguzi wa Kitabu. Yeye anaona kuwa lau ingelithibiti basi ingelikuwa ni yenye kuenea na imefanywa maalum kwa ufunguzi wa Kitabu.
[1] al-Bukhaariy (756) na Muslim (394).
[2] al-Bukhaariy katika ”al-Qiraa-ah khalf al-Imaam”, Abu Daawuud na Ahmad. Nzuri kwa mujibu wa at-Tirmidhiy na ad-Daaraqutwniy.
[3] 07:204
[4] Ibn Abiy Shaybah (1/97/1), Abu Daawuud, Muslim, Abu ´Awaanah na ar-Rawayaaniy katika ”al-Musnad” (1/119/24). Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (332) och (394).
[5] al-Albaaniy amesema:
”Ibn Abiy Shaybah (1/97/1), ad-Daraqutwniy, Ibn Maajah, at-Twahaawiy na Ahmad kupitia njia nyingi ambazo zilizoungana na zingine pasi na kutaja Maswahabah. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema kuwa Hadiyth ina nguvu, kama ilivyotajwa katika ”al-Furuu´” (2/48) ya Ibn ´Abdil-Haadiy. al-Buuswayriy amesahihisha baadhi ya njia zake. Nimelizungumzia hilo kwa kina na kuzitafiti njia hizo mbalimbali katika maandishi na vilevile katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (500).” (Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 87)
[6] Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 320-321
- Imechapishwa: 03/06/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 320-321
Imechapishwa: 03/06/2025
https://firqatunnajia.com/kisomo-cha-imamu-kinamtosheleza-mswaliji/