Swali: Kuna mwalimu mmoja anayesema kuwa filamu za kuigiza hazina neno. Amesimulia kisa kutoka kwa al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba walimuona bwana mmoja hatii vizuri wudhuu´ wake. Wakakubaliana bwana yule awe ndiye hakimu wao ni nani kati ya wawili hao anatawadha vyema. Wakatawadha na huku bwana yule anatazama. Bwana yule akatambua kuwa wawili hao wanatawadha vyema kuliko yeye na akazinduka juu ya kutia vizuri wudhuu´ wake. Unasemaje?

Jibu: Jibu ni kwa njia mbili:

1 – Thibitisha dalili kwanza. Ni kisa ambacho hakikuthibiti.

2 – Endapo kimesihi, walifanya hivo mara moja. Wao wamefanya ni taaluma. Wao hawafanyi hivo kutokana na kisa hicho. Ni kwa ajili ya kuwaigiliza wamagharibi. Filamu za kuigiza zinapingana na Shari´ah kikamilifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 251
  • Imechapishwa: 04/07/2022