Swali: Hadiyth kuhusu kipofu Ahl-ul-Bid´ah wameishikilia na ni utata kwao. Ni upi ufahamu wa Hadiyth hii na usahihi wake?

Jibu: Hadiyth kuhusu kipofu, ikiwa kweli imesihi, ndkipani yake hakuna kufanya Tawassul kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndani yake kuna kuomba du´aa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kipindi hicho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa yuhai na mbele yake. Kuomba du´aa kutoka kwa aliyehai na mbele yako ni jambo linafaa. Ni katika kufanya Tawassul kwa du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawana hoja yoyote ndani yake. Pamoja na kuwa cheni ya wapokezi wake imetiwa kasoro.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 78
  • Imechapishwa: 21/09/2018