Kipi kinachomlazimu anayeapiwa na rafiki yake kwa jina la asiyekuwa Allaah?

Swali: Je, inafaa kwa mtu kumuasi ambaye anaapa kwa kusema ”naapa kwa baba zangu kwamba utafanya kadhaa?”

Jibu: Analazimika kutubia kutokana na hilo. Kiapo hicho hakimlazimu mtu chochote, hakizingatiwi. Kiapo chake ni batili. Analazimika kutubia kutokana nacho. Hakuna chochote kinachomlazimu yule anayeapiwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24655/ماذا-يلزم-المحلوف-عليه-اذا-حلف-بالاباء
  • Imechapishwa: 21/11/2024