Swali: Je, Hadiyth inayosema:

“Anaacha chakula chake, kinywaji chake na matamanio yake kwa ajili Yangu.”[1]

si inafahamisha ya kwamba mfungaji anafungua kwa kutokwa na madhiy?

Jibu: Hapana, bali kinachokusudiwa na matamanio ni jimaa. Jengine ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akicheza michezo ya kimapenzi na wake zake akiwa na swawm. Isitoshe kujamiana ndiko kunakotoa matokeo ya matamanio.

[1] al-Bukhaariy (1894) na Muslim (1151) na (164) na tamko ni lake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 125
  • Imechapishwa: 02/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abi Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´