Kilichokusudiwa juu ya makatazo ya kutamani kukutana na adui

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msitamani kukutana na adui. Na mkikutana nao basi kuweni na subira.”

Jibu: Wanazuoni wameifasiri kwamba makatazo hapo yanahusu kutamani kukutana na adui kwa sababu ya kujiona, kujiamini nafsi kupita kiasi na mambo yanayofanana na hayo. Lakini mtu akitamani kukutana na adui kwa kutaka  jihaad au kutaka kufa shahidi katika njia ya Allaah, basi hilo linakuwa katika mlango wa jihaad. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehimiza jihaad na akahamasisha juu yake:

”Yule anayekufa bila kupigana vita wala bila kuizungumzisha nafsi yake juu ya kupigana vita, basi anakufa akiwa na tawi katika unafiki.”

Kwa hiyo katazo la kutamani si la jumla. Kinachokusudiwa ni kutamani kunakofuatana na majivuno, kiburi au kujiamini nafsi kupita kiasi. Lakini anayetamani kushiriki jihaad, basi kupigana katika njia ya Allaah na kukutana na adui wa Allaah, basi hakuna tatizo na hilo halimo ndani ya katazo hili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31685/ما-معنى-حديث-لا-تتمنوا-لقاء-العدو
  • Imechapishwa: 14/11/2025