Swali: Ni ipi tafsiri ya maneno Yake (Ta´ala):

كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“… kila pote kwa waliyokuwa nayo linafurahia.”[1]?

Jibu:

فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“Wakakatakata makundi na kutengana kuhusu dini yao, kila pote kwa waliyokuwa nayo linafurahia.”

Kila mmoja anaandika vitabu kuyanusuru madhehebu yake. Neno زُبُرًا linakusudia vitabu. Wameviandika kuhusu madhehebu yao. Kila mmoja ni mwenye kufurahia madhehebu yake hata kama yatakuwa yanapingana na dalili. Hawazirejelei dalili. Hii ndio maana yake. Hakuna neno kuandika vitabu, lakini ni lazima zirejelee dalili. Dalili ni lazima zifuatwe.

[1] 23:53

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (11) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14466
  • Imechapishwa: 10/10/2017