Kila alichokataza Mtume (´alayhis-Salaam) kina shari na wewe

Ukiona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo basi jua kufanya jambo hilo kuna shari na wewe. Usiulize kama amekataza kwa njia ya machukizo au uharamu, achana aliyokukataza sawa ikiwa ni kwa njia ya machukizo au uharamu. Usiiangamize nafsi yako! Msingi katika anayokataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  ni uharamu. Mpaka kuwepo dalili inayoonesha kuwa ni kwa njia ya machukizo ya kujitakasa. Vilevile akiamrisha jambo usiulize kuwa ni wajibu au sio wajibu, lifanye kwani ni kheri kwako kwa hali yoyote. Ikiwa ni wajibu umetimiza dhimma yako na umepata thawabu kwa hilo na ikiwa imependekezwa umepata pia thawabu. Katika hali hii unakuwa ni mwenye kumfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kikamilifu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/298)
  • Imechapishwa: 06/11/2024