Kikosi kikubwa cha wanazuoni kuhusu Tahiyyat-ul-Masjid

Swali: Hadiyth ya Zayd bin Aslam (Radhiya Allaahu ´anhaa) inayosema:

”Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakizungumza msikitini wakiwa hawana wudhuu´.”

swali: Je, inaweza kujengewa hoja ya kwamba swalah ya mamkuzi ya msiktii sio wajibu?

Jibu: Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa si wajibu kwa dalili isiyokuwa hii. Kama Hadiyth inayosema:

”Je, kuna nyenginezo zinazonilazimu, ee Mtume wa Allaah?” Akamwambia: ”Hapana, isipokuwa ukijitolea.””

Na yule aliye na hadathi ataswalije? Yeye ni mwenye udhuru. Mwenye hadathi ana udhuru. Ataswalije?

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24751/هل-تحية-المسجد-واجبة
  • Imechapishwa: 06/12/2024