Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:

”Allaah hushangazwa na kijana ambaye hana maovu ya ujana?”

Pia naomba ufafanuzi wa umri wa kukadiriwa unaoanzia kipindi cha ujana na unaomalizikia?

Jibu: Hii Hadiyth inajulikana sana, lakini sijui hali ya cheni yake hivi sasa. Maneno yake yana maana kwamba Allaah hushangazwa na kijana ambaye hana tabia za kijana zinazofanywa na vijana wengi, kama kuingia katika madhambi na makosa katika miaka yao ya mwanzo. Kwa maana tangu alipoanza kukua amekuwa katika ´ibaadah ya Allaah na utiifu Wake. Kwa maana nyingine hana maovu ya ujana, hana nyakati alizotoka katika mwongozo kwa sababu ya ujana. Huyo ndiye anayekuwa mahali pa kushangazwa na Allaah. Lakini kwa sasa sijui hali ya cheni ya Hadiyth kama ni nzuri au sivyo. Ni Hadiyth inayojulikana, lakini sasa siijui hali yake. Huenda nikaifuatilia – Allaah akitaka – na nikabainisha katika ijumaa ijayo – Allaah akitaka.

Swali: Kipindi cha ujana kinaanza lini na kuishia wapi?

Jibu: Dhahiri kinachokusudiwa ni mwanzo wa ujana wakati wa baleghe ndogo ya mabadiliko ya mwili, kisha baada ya kubaleghe. Kwa msemo mwingine miaka ya mwanzoni ya umri wake wakati wa baleghe na miaka inayoifuata.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/977/الحكم-على-حديث-ان-الله-يعجب-لشاب-ليس-له-صبوة
  • Imechapishwa: 23/12/2025