Kigezo cha usahihi wa kuielekea Ka´bah

ar-Raajihiy: Maana ya kuelekea sehemu iliyo wazi ya Ka´bah, kwa maana kwamba ikiwa mtu yuko juu ya mlima ulio juu ya Ka´bah – Je, swalah yake inasihi?

Ibn Baaz: Ndio, akiswali juu ya mlima unaozunguka Ka´bah kuelekea hewani kwake, swalah yake inasihi.

ar-Raajihiy: Je, kwa mtazamo huu inabidi kuelekea sehemu inayoonekana moja kwa moja?

Ibn Baaz: Si lazima, kilicho sahihi ni kwamba hapahitaji sehemu inayoonekana moja kwa moja.

ar-Raajihiy: Basi kwa maoni haya swalah haisihi?

Ibn Baaz: Hewa yake inatosha, kuelekea upande wake kunatosha.

Swali: Ikiwa ataswali karibu na Ka´bah, kisha baada ya kutoa salamu akagundua kwamba ameswali kinyume na Ka´bah, bali amepinda, naye alikuwa karibu nayo?

Jibu: Akiwa ameswali kinyume na Ka´bah, basi arudie swalah.

Swali: Vipi ikiwa amepinda kidogo tu?

Jibu: Upindaji mdogo unasamehewa.

Swali: Ikiwa atatembea kuelekea Ka´bah asigongane nayo?

Jibu: Swalah yake haisihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31619/ما-الضابط-في-صحة-استقبال-الكعبة-وهواىها
  • Imechapishwa: 08/11/2025