Swali: Nina mali katika benki fulani. Je, inajuzu nikubaliane na benki kwamba niifanye mali hii iwe ni mudhwaarabah baina yangu na benki; mimi nipate nusu ya faida na wao wapate nusu yake, na ikiwa itapata hasara pia basi hasara igawanywe nusu kwa nusu? Ni ipi suluhisho na njia ya hilo?
Jibu: Mudhwaarabah haina hasara juu ya mfanyakazi. Katika mudhwaarabah mfanyakazi ni mshirika katika faida, na hasara iko juu ya mmiliki wa mali. Kwa sababu mali ni amana mikononi mwa mfanyakazi. Ikiwa mfanyakazi hakufanya uzembe wala hakupunguza wajibu, basi hasara iko juu ya mmiliki wa mali. Faida hushirikishwa kwa nusu, kwa robo au kwa theluthi ikiwa biashara ni katika bidhaa maalum. Ikiwa ni katika benki kuna bidhaa maaluu, wanaweka katika magari maalum, wanaweka katika nyumba, katika mashamba kwa nusu, kwa theluthi au kwa robo. Hii ni mudhwaarabah. Inamlazimu amche Allaah katika hilo, alitunze, asilipuuzie na ailinde. Ikija faida, basi ni baina yao kwa mujibu wa sharti. Ikiwa haikuja faida, basi hasara iko juu ya mwenye mali. Haya ni ikiwa jambo lipo wazi. Lakini watu wa benki na watu wa ribaa hawaaminiki; huenda wakachanganya na mengine. Kwa hiyo inampasa afanye jambo hili na asiye mla ribaa, si pamoja na benki za ribaa bali na watu waaminifu ili aihifadhi mali yake isije ikamsaidia mla ribaa.
Swali: Vipi ikiwa atakubaliana na benki kuhusu hasara?
Jibu: Haisihi, ni sharti inayoenda kinyume.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1935/ضوابط-المضاربة-بين-العامل-وصاحب-المال
- Imechapishwa: 28/12/2025
Swali: Nina mali katika benki fulani. Je, inajuzu nikubaliane na benki kwamba niifanye mali hii iwe ni mudhwaarabah baina yangu na benki; mimi nipate nusu ya faida na wao wapate nusu yake, na ikiwa itapata hasara pia basi hasara igawanywe nusu kwa nusu? Ni ipi suluhisho na njia ya hilo?
Jibu: Mudhwaarabah haina hasara juu ya mfanyakazi. Katika mudhwaarabah mfanyakazi ni mshirika katika faida, na hasara iko juu ya mmiliki wa mali. Kwa sababu mali ni amana mikononi mwa mfanyakazi. Ikiwa mfanyakazi hakufanya uzembe wala hakupunguza wajibu, basi hasara iko juu ya mmiliki wa mali. Faida hushirikishwa kwa nusu, kwa robo au kwa theluthi ikiwa biashara ni katika bidhaa maalum. Ikiwa ni katika benki kuna bidhaa maaluu, wanaweka katika magari maalum, wanaweka katika nyumba, katika mashamba kwa nusu, kwa theluthi au kwa robo. Hii ni mudhwaarabah. Inamlazimu amche Allaah katika hilo, alitunze, asilipuuzie na ailinde. Ikija faida, basi ni baina yao kwa mujibu wa sharti. Ikiwa haikuja faida, basi hasara iko juu ya mwenye mali. Haya ni ikiwa jambo lipo wazi. Lakini watu wa benki na watu wa ribaa hawaaminiki; huenda wakachanganya na mengine. Kwa hiyo inampasa afanye jambo hili na asiye mla ribaa, si pamoja na benki za ribaa bali na watu waaminifu ili aihifadhi mali yake isije ikamsaidia mla ribaa.
Swali: Vipi ikiwa atakubaliana na benki kuhusu hasara?
Jibu: Haisihi, ni sharti inayoenda kinyume.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1935/ضوابط-المضاربة-بين-العامل-وصاحب-المال
Imechapishwa: 28/12/2025
https://firqatunnajia.com/kigezo-cha-mudhwaarabah-baina-ya-mfanyakazi-na-mwenye-mali/