Kigezo cha damu nyingi na ndogo

Swali: Je, damu kidogo kwenye nguo husamehewa?

Jibu: Ndiyo, damu kidogo husamehewa.

Swali: Kiwango chake ni kipi?

Jibu: Ni kiasi ambacho mwenyewe anaona kuwa ni kidogo. Kwa kiwango anavyoona yeye, kama haioni kuwa ni kitu kikubwa.

Swali: Hakuna tofauti kati ya damu inayochuruzika na isiyochuruzika?

Jibu: Hakuna tofauti, ni kwa mujibu wa jinsi anavyoona mwenyewe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31600/ما-حد-الدم-اليسير-في-الثياب-وما-حكمه
  • Imechapishwa: 07/11/2025